Covid-19: Watu 480 wapatikana na corona, 5 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya  imerekodi visa 480 vipya vya maambukizi  ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,120 katika muda wa saa 24 zilizopita
  • Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 190,183 kutoka kwa sampuli 2,028,927
  • Katika visa hivi vipya,459 ni raia wa Kenya huku 21 akiwa raia wa kigeni,245 ni wa kiume na  ni 235 wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya  imerekodi visa 480 vipya vya maambukizi  ya COVID-19 kutoka kwa sampuli 5,120 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Kufikia sasa Kenya imesajili jumla ya visa 190,183 kutoka kwa sampuli 2,028,927.

Katika visa hivi vipya,459 ni raia wa Kenya huku 21 akiwa raia wa kigeni,245 ni wa kiume na  ni 235 wanawake.

Mgonjwa mwenye umri wa chini ana miezi 2 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Asilimia ya maambukizi ya corona imefika sasa 9.4%.

Watu 148 wamepona virusi vya corona,81 walipona wakiwa nyumbani huku 67 wakipona wakiwa katika hospitali mbali mbali, na kufikisha idadi jumla ya 180,080 ya watu waliopona.

Hata hivyo habari za kuhuzunisha ni kwamba watu 5 wameaga dunia kutokana na maambukizi kufikisha 3,737  watu waliofariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.

Jumla ya wagonjwa 1,075 wamelazwa katika vituo mbali mbali vya afya , huku 4,486 wakiuguzwa nyumbani.

Wagonjwa 121 wamo katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).