Jubilee yashinda kiti cha wadi ya Muguga

Muhtasari

• Mgombeaji waJubilee alizoa Jumla ya kura 4,089 dhidi ya kura 4,062 za mpinzani wake wa karibu na kushinda kwa kura 27 pekee.

Mgombeaji wa Jubilee Joseph Githinji
Mgombeaji wa Jubilee Joseph Githinji

Mung'ara Joseph Githinji wa chama tawala cha Jubilee ameibuka mshindi wa kiti cha wadi ya Muguga katika kaunti ya Kiambu.

Githinji ambaye alikuwa mgombeaji wa chama tawala cha Jubilee alishinda kinyang'anyiro hicho katika uchaguzi mdogo ulioandaliwa siku ya Alhamisi kwa ushindi finye mno wa asilimia 50 dhidi ya mpinzani wake wa UDA, Thumbi Peter Kamau aliyepata asilimia 49.

Mgombeaji waJubilee alizoa Jumla ya kura 4,089 dhidi ya kura 4,062 za mpinzani wake wa karibu na kushinda kwa kura 27 pekee.

Mumbi Joseph Gichau alimaliza wa tatu kwa kura 49 huku Mugo Peter Njoroge akimaliza wa nne kwa kura 32.

Kulingaqnba na takwimu za tume huru ya uchaguzi na mipaka jumla ya kura 8,342 zilipigwa huku kura 110 zikiharibika.Ni asilimia 45.40 ya wapiga waliojitokeza kupiga kura.

Kiti cha wadi ya Muguga kilisalia wazi kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi wadi Eliud Ngugi aliyefariki mwezi Machi mwaka huu kutokana na vurusi vya Covid-19 alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya chuo Kikuu cha Kenyatta.