Matiang'i atangaza Jumanne wiki ijayo kuwa sikukuu

Sikukuu ya Eid-Ul-Adha ambayo husherehekewa kila mwaka ni sikukuu ya dhabihu na huwa ya kuadhimisha kujitolea kwa Ibrahimu kuutoa mwanawe kafara.

Muhtasari

•Matiang'i alichapisha siku hiyo kuwa sikukuu ya kuadhimisha Idd-Ul Adha kwenye gazeti rasmi la serikali.

Image: HISANI

Waziri wa maswala ya ndani  Fred Matiang'i ametangaza siku ya Jumanne wiki ijayo, Julai 20 kuwa sikukuu.

Matiang'i alichapisha siku hiyo kuwa sikukuu ya kuadhimisha Idd-Ul Adha kwenye gazeti rasmi la serikali.

Sikukuu ya Eid-Ul-Adha ambayo husherehekewa kila mwaka ni sikukuu ya dhabihu na huwa ya kuadhimisha kujitolea kwa Ibrahimu kuutoa mwanawe kafara.