Watu 13 wafariki, 11 wajeruhiwa vibaya kwenye mlipuko wa lori la mafuta Siaya

Lori hilo la mafuta lilipoanguka mafuta yalianza kumwagika na wanakijiji wakatokea mbio kuyachota.

Muhtasari

•Inaripotiwa kuwa  lori  hilo liligongana na lori lingine ambalo lilikuwa limebeba maziwa kisha  kuvingirika na kumwaga mafuta mwendo wa saa tano kasorobo.

•Mili ya watu 12 ambao walikuwa wameteketea hadi kuaga ilipatikana huku wengine 11 ambao waliugua majeraha mabaya wakikimbizwa katika hospitali ya Yala.

Image: HISANI

Takriban watu 13 walifariki na wengine 11 walijeruhiwa vibaya  Jumamosi usiku wakati lori  la mafuta lililipuka na kuteketea katika kijiji cha Malanga kilicho kwenye barabara ya kutoka Kisumu kuelekea Busia.

Inaripotiwa kuwa  lori  hilo liligongana na lori lingine ambalo lilikuwa limebeba maziwa kisha  kuvingirika na kumwaga mafuta mwendo wa saa tano kasorobo.

Kamanda wa polisi maeneo ya Yala, Charles Chacha alisema kuwa dereva wa lori  la maziwa alikuwa anajaribu kuzuia  vichwa vya lori hizo kugongana  ila akaligonga upande lile la mafuta ambalo lilikuwa linatoka Kisumu.

Lori hilo la mafuta lilipoanguka mafuta yalianza kumwagika na wanakijiji wakatokea mbio kuyachota. Baada ya kipindi kifupi lori hilo lililipuka kwa kishindo.

Mili ya watu 12 ambao walikuwa wameteketea hadi kuaga ilipatikana huku wengine 11 ambao waliugua majeraha mabaya wakikimbizwa katika hospitali ya Yala.

Kulingana na OCPD wa maeneo hayo, iliwachukua wazima moto masaa matatu kuweza kudhibiti moto ule