Raila asihi Wakenya kutumia tukio la mlipuko wa tangi lililoua watu 13 Gem kama funzo

Amewaomba Wakenya kutoroka kutoka kwenye eneo la tukio iwapo wakati wowote ajali ianyohusisha lori la mafuta inajitokeza.

Muhtasari

•Mwanasiasa huyo alikumbusha Wakenya tukio kama hilo lililotokea 1998 maeneo ya Sidindi ambapo  watu 33 walipoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa vibaya baada ya lori la mafuta kuanguka kwa shamba la mahindi

•Mnamo Januari mwaka wa 2009, watu 113  waliteketea hadi kifo na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa vibaya  baada ya tangi la mafuta kulipuka walipokuwa wanachota mafuta maeneo ya Molo.

Baki la tangi la mafuta ambalo lililipuka Gem
Baki la tangi la mafuta ambalo lililipuka Gem
Image: DICKENS WESONGA

Kinara wa ODM Raila Amolo Odinga amewasihi Wakenya kujifunza kutokana na tukio la mlipuko wa tangi ambalo lilsababisha maafa ya watu 13 na kujeruhi wengine 31 usiku wa Jumamosi maeneo wa Gem.

Kupitia ujumbe ambao aliandika mitandaoni Jumatatu asubuhi, Raila amesema kuwa anatumai kuwa hilo ni tukio la mwisho ambapo Wakenya watang'angana kuchota mafuta baada ya lori kuanguka.

Amewaomba Wakenya kutoroka kutoka kwenye eneo la tukio iwapo wakati wowote ajali ianyohusisha lori la mafuta inajitokeza.

"Tunapoomboleza na kutafakari, natumai kuwa hii ni mara ya mwisho ambapo watu wetu wanakufa kutokana na kung'angania mafuta lori la mafuta linapoanguka. Natumai kuwa wakati mwingine watu watakimbia, sio kuelekea kwa tukio ila kutoroka." Raila alisema.

Raila alifariji familia za waliopoteza maisha yao na kutakia afweni ya haraka wale ambao waliummia kufuati ajali hiyo.

Mwanasiasa huyo alikumbusha Wakenya tukio kama hilo lililotokea 1998 maeneo ya Sidindi ambapo  watu 33 walipoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa vibaya baada ya lori la mafuta kuanguka kwa shamba la mahindi.

Mnamo Januari mwaka wa 2009, watu 113  waliteketea hadi kifo na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa vibaya  baada ya tangi la mafuta kulipuka walipokuwa wanachota mafuta maeneo ya Molo.

Miezi tano baadae, tukio kama hilo lilishuhudiwa katika kijiji cha Kapokyek upande wa Kericho ambapo watu wanne walipoteza maisha yao na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa walipokuwa wanachota mafuta.