Makali ya COVID 19: Visa vipya 618, Vifo 17 vyaripotiwa; 1222 wamelazwa hospitani

Mtoto wa miezi sita na mkongwe wa miaka 103 ni baadhi ya waliopatikana na virusi vya Corona.

Muhtasari

•Kenya imeandikisha wagonjwa wapya 618 wa maradhi ya COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 5507  waliopokea vipimo ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

•Watu 290 waliweza kupata afueni ambapo  261 kati yao walikuwa wamelazwa hosspitali ilhali 29 waliponea manyumbani.  Kufikia sasa watu 183,211 waliowahi kuugua COVID 19 nchini wameripotiwa kupona.

Image: HISANI

Kenya imeandikisha wagonjwa wapya 618 wa maradhi ya COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 5507  waliopokea vipimo ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Kati ya 618 hao, 38 ni raia wa kigeni ilhali wengine wote ni Wakenya. Asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 11.2%.

Mtoto wa miezi sita na mkongwe wa miaka 103 ni baadhi ya waliopatikana na virusi vya Corona.

Tangu kuanza kwa maambukizi ya virusi hivyo nchini mapema mwaka uliopita, Kenya imeandikisha wagonjwa 193,807 kutoka kwa sampuli ya watu 2.064,700 waliowahi kupimwa.

Hivi leo kaumti ya Nairobi imeandikisha wagonjwa wengi zaidi ikiripoti visa 272 ikifuatwa na Mombasa 52, Kiambu 41, Nakuru 30, Uasin Gishu 24, Migori 23, Busia 19, Nandi 17, Kirinyaga  12, Kilifi 11, Kitui 10, Murang'a 10.

Kajiado, Kericho, Kisumu, Machakos, Siaya, Vihiga, Garisa, Taita Taveta, Turkana, Homabay, Nyandarua, Meru, Embu, Bungoma, Kakamega, Kisii, Nyamira, Nyeri, Bomet, Laikipia na makueni ziliandikisha visa chini ya 10 kila kaunti.

Watu 290 waliweza kupata afueni ambapo  261 kati yao walikuwa wamelazwa hosspitali ilhali 29 waliponea manyumbani.  Kufikia sasa watu 183,211 waliowahi kuugua COVID 19 nchini wameripotiwa kupona.

La kusikitisha ni kuwa vifo 17 vimeripotiwa na kufikisha idadi ya walioaga kutokana na virusi hivyo kuwa 3800.

Wagonjwa 1222 wanaendelea kupokea matibabu hospitalini huku wengine 4339 wakiangaliwa manyumbani.

Wagonjwa 139 wamelazwa kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi huku 273 wengine wakiwa wanaongezewa hewa.

CHANJO YA CORONA

Kufikia leo watu 1,040,317 wameweza  kupokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya maambukizi ya COID 19 ilhali 595, 124 pekee kati yao ndio wameweza kupata dozi zote mbili.