Wanne waaga kwenye ajali ya kuhofisha Mlolongo

Inadaiwa kuwa wanne hao waliaga papo hapo baada ya matatu waliyokuwa wameabiri kugongana na trela lililokuwa limesimama kando ya kituo cha petroli.

Muhtasari

•Matatu hiyo ya MAPTRA SACCO,  namba ya usajili KCN 289P ilikuwa inaelekea Nairobi wakati ajali ilipotokea dakika chache kabla ya saa kumi na moja.

Matatu iliyoganga trela
Matatu iliyoganga trela
Image: GEORGE OWITI

Habari na George Owiti

Watu wanne wamefariki kufuatia ajali mbaya  iliyotokea maeneo ya Mlolongo kwenye barabara kuu ya kutoka Nairobi kuelekea Mombasa asubuhi ya kuamkia Jumatano.

Akithibitisha ajali hiyo, Kamishna msaidizi wa kaunti ya Machakos eneo la Mlolongo Dennis Ongaga amesema kuwa wanne hao waliaga papo hapo baada ya matatu waliyokuwa wameabiri kugongana na trela lililokuwa limesimama kando ya kituo cha petroli.

Matatu hiyo ya MAPTRA SACCO,  namba ya usajili KCN 289P ilikuwa inaelekea Nairobi wakati ajali ilipotokea dakika chache kabla ya saa kumi na moja.

Mengine yatafuata...