Makali ya corona: Watu 15 wameaga dunia,801 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 801 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,850 chini ya saa 24 zilizopita
  • Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 195,111 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.7%
Image: HISANI

Watu 801 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 5,850 chini ya saa 24 zilizopita.

Visa hivyo sasa vinafikisha maambukizi ya Corona nchini Kenya hadi 195,111 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 13.7%.

Kulingana na wizara ya afya watu 15 wameaga dunia kutokana na viruis vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 3,826 ya walioaga dunia.

Jumla ya wagonjwa 293 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 184,461, 322 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 159 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,248 ambao wamelazwa hospitalini,3,862 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 135 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 1,648,869.