Maafisa wa KWS wanasa simba aliyesababisha drama Rongai

Simba huyo alirejeshwa kwenye mbuga la wanyama la Nairobi baada ya kumkamata

Muhtasari

•Wakazi walimpata simba huyo akiwa amejificha kwenye ushoroba wa nyumba moja karibu na Tuskys Jumatano asubuhi.

•Polisi na maafisa wa KWS walifika katika eneo hilo na kufurusha umati mkubwa wa watu waliokuwa wamejumuika kujionea mnyama huyo.

Image: HISANI

Maafisa wa KWS wamekamata simba aliyetoka nje ya mbuga la wanyama la Nairobi na kusababisha drama kubwa maeneo ya Ongata Rongai.

Wakazi walimpata simba huyo akiwa amejificha kwenye ushoroba wa nyumba moja karibu na Tuskys Jumatano asubuhi.

Polisi na maafisa wa KWS walifika katika eneo hilo na kufurusha umati mkubwa wa watu waliokuwa wamejumuika kujionea mnyama huyo.

Haijabainika wazi wakati simba huyo aliweza kutoka nje ya mbuga la Nairobi alikokuwa akiishi.

Maafisa wa KWS walimrejesha kwenye mbuga hilo baada ya kumkamata.

Hii sio mara ya kwanza ripoti za simba kutoka nje ya mbuga la Nairobi kutokea. Tukio kama hilo lilishuhudiwa mwaka wa 2016 na 2019.