Raila Odinga apokea chanjo ya corona

Muhtasari
  • Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amepokea chanjo dhidi ya virusi vya covid-19 siku ya Ijumaa, JUlai 30
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter kigogo huyo aliwahimiza wakenya ambao hawajapokea chanjo hiyo kuipokea
Raila Odinga
Image: Twitter

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amepokea chanjo dhidi ya virusi vya covid-19 siku ya Ijumaa, JUlai 30.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter kigogo huyo aliwahimiza wakenya ambao hawajapokea chanjo hiyo kuipokea.

Mwezi wa Machi mwaka huu Raila alipatikana na virusi vya corona na kulazwa hospitalini, baada ya kugunduliwa kuwa na virusi hivyo.

Kulingana na baadhi ya wandani wake huenda kiongozi huyo wa ODM alipata virusi hivyo akiwa katika ziara ya kupigia debe mchakato wa BBI katika kanda ya Pwani.

"Leo mchana nimepata chanjo ya AstraZeneca Covid-19.Kwa kuwa nimeathiriwa na virusi hivi hatari ninawahimiza wale wote ambao wanastahili kupata chanjo wapate chanjo.

Natoa wito kwa serikali ifanye mipango thabiti ya chanjo ya wingi mara tu chanjo zitakapotua na, pia ninahimiza Wakenya wajisikie huru kuchukua jab.

Tutashinda virusi!" Aliandika Raila.

Haya yanajiri wakati, kufikia Alhamisi jumla ya watu waliopokea chanjo ya corona ikifikia 1,712,550.