Covid-19: Watu 32 waaga dunia,1,571 wapatikana na corona,4,497 wapona

Muhtasari
  • Watu 1,571 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,065 chini ya saa 24 zilizopita
  • Idadi jumla ya watu walipatwa na corona nchini imefika208,262 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 17.3%
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 1,538ni wakenya ilhali 33 ni raia wa kigeni,846 ni wanaume huku 725 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 1,571 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,065 chini ya saa 24 zilizopita.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika208,262 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 17.3%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 1,538ni wakenya ilhali 33 ni raia wa kigeni,846 ni wanaume huku 725 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.

Kulingana na wizara ya afya watu 32 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,057 ya walioaga dunia.

Aidha watu 4,497 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 195,685, 4,335 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 162 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,618 ambao wamelazwa hospitalini,4,187 wamejitenga nyumbani.

Pia kuna wagonjwa 112 kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).