Mshukiwa mkuu katika mauaji ya vijana wanne Kitengela atiwa mbaroni

Ole Mungai alihusishwa na mauaji ya vijana hao baada ya upelelezi wa DCI kuthibitisha kuwa alikuwa katika eneo la tukio.

Muhtasari

•Maafisa wa DCI wamesema kuwa Benson Melonyie Ole Mungai, 40, alikamatwa jana jioni (Agosti 17) akiwa mafichoni yake mjini Kitengela.

•Inadaiwa kuwa Mungai ndiye aliratibu mauaji ya  Fredrick Mureithi (30) Victor Mwangi (25), Mike George (29)  na Nicholas Musa (28).

Mike George 29, Fredrick Mureithi 22, Victor Mwangi 26, Nicholas Musa 28 na pikipiki zao zilizochomwa Kitengela
Mike George 29, Fredrick Mureithi 22, Victor Mwangi 26, Nicholas Musa 28 na pikipiki zao zilizochomwa Kitengela
Image: KURGAT MARINDANY

Mshukiwa mkuu katika mauaji ya vijana wanne wa familia moja ambao walipoteza maisha ya usiku wa Agosti 8 wakiwa  Kitengela amekamatwa.

Maafisa wa DCI wamesema kuwa Benson Melonyie Ole Mungai, 40, alikamatwa jana jioni (Agosti 17) akiwa mafichoni yake mjini Kitengela.

Inadaiwa kuwa mshukiwa amekuwa akijificha pale tangu alipopanga na kutekeleza mauaji yale takriban wiki moja iliyopita.

Ole Mungai alihusishwa na mauaji ya vijana hao baada ya upelelezi wa DCI kuthibitisha kuwa alikuwa katika eneo la tukio.

Inadaiwa kuwa Mungai ndiye aliratibu mauaji ya  Fredrick Mureithi (30) Victor Mwangi (25), Mike George (29)  na Nicholas Musa (28).

Polisi wanamzuilia mshukiwa ili kusaidia katika uchunguzi huku wapelelezi  wakiendelea kuwasaka washukiwa wengine.