Mfahamu kiongozi wa kundi la Taliban

Mullah Abdul Ghani Baradar: Mfahamu kiongozi wa kundi la Taliban

Muhtasari

• Alipanda na kuwa mtu muhimu wa kundi hilo baada ya Taliban kufurushwa nchini Afghinistan na Marekani 2001.

• Alikamatwa kupitia uvamizi wa pamoja uliotekelezwa na Marekani wakishirikiana na Pakistan , kusini mwa mji wa Pakistan wa Karachi mnamo mwezi Februari 2010.

Image: GETTY IMAGES

Mullah Abdul Ghani Baradar ni mmoja ya watu wanne walioanzisha kundi la Taliban nchini Afghanistan 1994.

Alipanda na kuwa mtu muhimu wa kundi hilo baada ya Taliban kufurushwa nchini Afghinistan na Marekani 2001.

Alikamatwa kupitia uvamizi wa pamoja uliotekelezwa na Marekani wakishirikiana na Pakistan , kusini mwa mji wa Pakistan wa Karachi mnamo mwezi Februari 2010.

Hakusikika tena hadi mwaka 2012 wakati jina lake lilipoorodheshwa katika orodha ya wafungwa wa Taliban ambao serikali ya Afghan ilitaka kuwaachilia ili kuvutia mazungumzo ya amani.

Pakistan baadaye ilimuachilia Baradar tarehe 21 Septemba lakini haijulikani alienda kuishi wapi.

Wakati wa kukamatwa kwake alidaiwa kuwa naibu wa kiongozi wa kidini wa kundi hilo Mullah Mohammad Omar, na mmoja ya makomanda aliyemuamini sana.

Viongozi wakuu wa Afghanistan walikuwa na matumaini kwamba mtu kama yeye angeweza kulishawishi kundi la Taliban kufanya mazungumzo na serikali ya Kabul - mpango wa serikali uliokuwa na malengo ya udhibiti baada ya vikosi vya Nato kuondoka nchini humo 2014.

Ni mmoja wa viongozi wa kundi hilo ambaye amekuwa akipenda kufanyika kwa mazungumzo na Marekani pamoja na serikali ilioondolewa ya Afghanistan.

Mthibiti wa fedha

Baada ya kuwa mmoja ya waanzislishi wa kundi la Taliban 1994, Mullah Baradar alijipatia kazi ya kuwa kamanda wa mikakati ya kijeshi.

Alidaiwa kusimamia operesheni za kila siku za kundi hilo na ufadhili wake.

Alisimamia majukumu muhimu katika vita vyote vikuu nchini Afghanistan, na kusalia kamanda mkuu wa kundi la Taliban katika eneo la magharibi la Herat pamoja na Kabul.

Wakati ambapo Taliban walifurushwa, alikuwa naibu waziri wa ulinzi. Mkewe ni dadaake Mullah Omar.

Alikuwa akifanya mashambulizi makali dhidi ya vikosi vya serikali ya Afghan , alisema afisa mmoja wa Afghan ambaye hakutaka jina lake litajwe wakati wa kukakamtwa kwake.

Mullah Baradar, kama viongozi wengine wa Taliban , alilengwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa , ambalo lilimshirikisha kupiga tanji mali ya kundi hilo, kulipiga marufuku kusafiri na kuzuia kundi hilo kuuziwa silaha.

Kabla ya kukamatwa kwake 2010, alitoa taarifa kadhaa kwa umma. Lakini mojawapo ya taarifa hizo ilikuwa 2009 mwezi Julai, ambapo alirushiana cheche za maneno la gazeti la Newsweek.

Alipoulizwa kujibu kuhusu kuongezeka kwa idadi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, alisema kwamba Taliban inataka kuisababishia hasara kubwa Marekani.

Mullah Baradar alikamatwa katika mji wa kusini wa Karachi
Mullah Baradar alikamatwa katika mji wa kusini wa Karachi
Image: GETTY IMAGES

Pia aliapa kuendeleza Jihad hadi maadui zao watakapoondoka katika ardhi yao.

Alisema kwamba Mullah Omar alikuwa katika hali nzuri na kuongoza vita dhidi ya muungano wa Kaskazini huku akikana madai kwamba viongozi wa Taliban walikuwa wamepiga kambi Pakistan.

Alipoulizwa kuhusu masharti yao ya kuleta amani, alijibu: Masharti ya msingi ni kuondoka kwa vikosi vya kigeni katika ardhi ya Afghanistan.

Kulingana na polisi ya kimataifa interpol , Mullah Baradar alizaliwa katika Kijiji cha Weetmak wilayani Dehrawood katika mkoa wa Uruzgan Afghanistan 1968.

Lakini pia anatambulika kutoka kwa kabila la Durrani kutoka tawi la Popalzai , sawa na lile kabla la aliyekuwa rais wa zamani wa Afghanistan Hamid Karzai.

Aliripotiwa kuwa karibu na nduguye rais Karzai , Ahmad Wali Karzai, ambaye ndiye aliyekuwa mkuu wa baraza la mkoa wa Kandahar kutoka 2005 hadi alipouawa mwezi Julai 2011.