Video: Rayvanny na gavana Mutua kuzindua ngoma

Muhtasari

• Rayvanny na gavana Mutua watazindua wimbo wa birthday 

Gavana wa Machakos Alfred Mutua na mwanamuziki wa bongo Rayvanny walipozuru studio za Radio Jambo, mnamo Agosti 20/2021
Gavana wa Machakos Alfred Mutua na mwanamuziki wa bongo Rayvanny walipozuru studio za Radio Jambo, mnamo Agosti 20/2021

Star wa bongo Ryavanny yuko nchini Kenya kwa show ya kukata na shoka mnano Agosti 22 kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake ambayo pia itakuwa siku ya kuzaliwa kwa gavana wa Machakos Alfred Mutua. 

Katika mahojiano ya kipekee gavana Mutua ambaye amekuwa akitamba kwenye mitandao ya kijamii baada ya ripoti kuibuka kuhusu kutengana kwake na mkewe Lilian, alisema tamasha hilo la siku ya Jumapili litahudhuriwa tu na watu wachache waalikwa.

Gavana Mutua alisema sababu ya kualika watu wachache ni kuambatana na  kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi ya vurusi vya Corona. 

Wawili hao ambao walikwepa swali kuhusu umri wao walisema kwamba siku hiyo watazindua wimbo mpya wa 'birthday'.