Covid-19: Watu 1,457 wapona corona,31 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 932 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,424 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 909 ni wakenya ilhali 23 ni raia wa kigeni,473 ni wanaume huku 459 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa 932 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,424 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 909 ni wakenya ilhali 23 ni raia wa kigeni,473 ni wanaume huku 459 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 233,801 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 9.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,352,240.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 11, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 31 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,666 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 1,457 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 218,228, 1,309 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 148 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,953 ambao wamelazwa hospitalini, 8,022 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 161 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,693,039