Taliban wadhibiti uwanja wa ndege baada ya Marekani kuondoka

Muhtasari

• Picha mpya zimeibuka za Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, baada tu ya ndege ya Marekani kuondoka.

Image: EPA

Picha mpya zimeibuka za Taliban wakiingia kwenye uwanja wa ndege wa Kabul, baada tu ya ndege ya Marekani kuondoka.

Mwandishi wa gazeti la Los Angeles Times Nabih Bulos, aliwafuatilia wapiganaji wa Taliban walipokuwa wakilitazama eneo ambalo kulikuwa na ndege iliyoachwa na vikosi vya Marekani

‘’Tuko hapa na Taliban wakati wakiingia uwanjani ikiwa ni dakika chache zimepita tangu sehemu ya eneo hili la uwanja wa ndege lilipokuwa likidhibitiwa na Marekani.Sasa wamechukua udhibiti,’’ alisema mbele ya kamera.

Video nyingine zinaonesha wapiganaji wa Taliban wakifyatua risasi angani ikiwa ishara ya kushangilia, walishangilia na kupiga picha, na kuzunguka katika eneo lote la uwanja.