Makali ya corona: Watu 1,018 wapatikana na corona,13 wameaga dunia

Muhtasari
  • Idadi  hii imefikisha jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa nchini kuwa 236,881 kutoka kwa vipimo 2,380,918 ambavyo vimefanywa tangu kuingia kwa virusi vya Corona nchini
  • Asilimia ya maambukizi  kwa sasa imesimamia 10.9%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Wizara ya afya leo hii imetangaza visa vipya 1,018 vya wagonjwa wa COVID-19 kutoka kwa sampuli ya watu 9,347 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliyopita.

Idadi  hii imefikisha jumla ya visa vilivyowahi kuripotiwa nchini kuwa 236,881 kutoka kwa vipimo 2,380,918 ambavyo vimefanywa tangu kuingia kwa virusi vya Corona nchini.

Asilimia ya maambukizi  kwa sasa imesimamia 10.9%.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 995 ni wakenya ilhali 23 ni raia wa kigeni,496 ni wanaume huku 522 wakiwa wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 11, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 103.

Aidhawatu 633 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 224,270.,  493wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 140 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 13 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,739 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa  1,866 ambao wamelazwa hospitalini, 4,988 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 160 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,792,309.