Covid-19:Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,809,389,watu 1,001 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 1,001 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,065 chini ya saa 24 zilizopita
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa 1,001 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 9,065 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 988 ni wakenya ilhali 13 ni raia wa kigeni,504 ni wanaume huku 497 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 238,852 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.0%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,397,923.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 4, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 110.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 11 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,757 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 1,155 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 226,037.

1,001 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 154 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,867 ambao wamelazwa hospitalini, 5,190 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 135 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,809,389.