Corona:Watu 840 wapatikana na corona,1,237 wapona,21 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 239,6692 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 10.3%
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS
MAJARIBIO YA CHANJO: Chanjo mpya ya Pfizer na BioNTech ina kinga ya asilimia 90 Picha: REUTERS

Kenya imesajili visa 840 vipya vya maambukizi ya Covid-19  siku ya Jumamosi kutoka kwa sampuni 8,129 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 812 ni wakenya ilhali 28 ni raia wa kigeni,438 ni wanaume huku 402 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 239,6692 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 10.3%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,406,052

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 2, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 21 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,778 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 1,237 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 227,274.

1,104 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 133 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,863 ambao wamelazwa hospitalini, 4,937 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 147 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).