Makali ya corona:Watu 480 wapatikana na corona,809 wapona,8 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 240,172 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.5%
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,411,720
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka 1, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya imesajili visa 480 vipya vya maambukizi ya Covid-19  siku ya Jumapili kutoka kwa sampuni 5,668 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 448 ni wakenya ilhali 32 ni raia wa kigeni,226 ni wanaume huku 254 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 240,172 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.5%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,411,720.

Mgonjwa wa umri wa chini ana mwaka 1, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 98.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 8 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,786 ya walioaga dunia.

Vile vile watu 809 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 228,083

703 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 106 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,829 ambao wamelazwa hospitalini, 4,994 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 155 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).