Covid-19: Watu 258 wapatikana na corona huku9 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Watu 258 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,137 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 241 ni wakenya ilhali 17 ni raia wa kigeni,142 ni wanaume huku 116 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Watu 258 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 3,137 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 241 ni wakenya ilhali 17 ni raia wa kigeni,142 ni wanaume huku 116 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 240,430 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 8.2%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,414,857.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miezi 3, huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 102.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 9 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,795 ya walioaga dunia.

Aidha watu 923 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 229,006, 861 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 62 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,825 ambao wamelazwa hospitalini, 4,546 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 151 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 2,870,392.