34 waaga dunia huku 501 wakiambukizwa Covid-19

Muhtasari

• Vifo vya watu vimeongezeka hadi 4,864 baada ya wagonjwa wengine 34 kuaga.

• Kagwe alisema kuwa kuna wagonjwa 1,752 wanaolazwa kwa sasa katika vituo vya afya nchini kote, huku 4,864 wakiwa nyumbani chini ya mpango wa kutunzwa Nyumbani.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe

Kenya siku ya Alhamisi ilirekodi visa vipya 501 vya Covid-19, na kufikisha jumla ya visa 242,284, vya Korona nchini, waziri Mutahi Kagwe alisema.

Waziri katika taarifa alithibitisha kuwa hii ilikuwa kutoka kwa sampuli 6,879, ikirekodi kiwango cha maambukizi cha asilimia 7.3.

Jumla watu 2,436,216 wamepimwa virusi hivyo nchini.

Vifo vya watu vimeongezeka hadi 4,864 baada ya wagonjwa wengine 34 kuaga kutokana na ukakuzi wa baadaye wa sajili katika hospitali mbali mbali katika miezi ya Julai, Agosti na Septemba.

Kagwe alisema kuwa kuna wagonjwa 1,752 wanaolazwa kwa sasa katika vituo vya afya nchini kote, huku 4,864 wakiwa nyumbani chini ya mpango wa kutunzwa Nyumbani.

Wagonjwa wengine 163 wako katika Kitengo cha Huduma Mahututi, 117 kati yao wako kwenye msaada wa upumuaji na 40 kwenye oksijeni ya kuongezea.

Wagonjwa wengine 671 wako kwa oksijeni ya ziada, 617 kati yao katika wadi za jumla na 54 katika Vitengo vya HDU.

Wakati huo huo, wagonjwa 312 wamepona ugonjwa huo, 190 kutoka vituo vya afya nchini kote huku 122 wakipona kutoka nyumbani.

Jumla ya watu 230,407 kati yao 186,825 wametoka kwa mpango wa Huduma ya Kutunzwa Nyumbani na Kutengwa, wakati 43,582 ni kutoka vituo vya afya.