Jimi Wanjigi amtunuku Eric Omondi gari la kifahari

Muhtasari

• Jimi alisema gari hilo la bei ghali litatumika na Eric kwenda katika kila pembe ya akieneza ujumbe wa bwenyenye huyo.

Eric Omondi na Jimi Wanjigi Picha: HISANI
Eric Omondi na Jimi Wanjigi Picha: HISANI

Mcheshi Eric Omondi amepewa zawadi ya gari aina ya Chrysler na mwanasiasa Jimi Wanjigi.

Kwenye video aliyopakia kwenye akaunti yake ya Instagram, Omondi alikuwa na mfanyibiashara Jimi akipokezwa ufunguo wa gari hilo.

Jimi alisema gari hilo la bei ghali litatumika na Eric kwenda katika kila pembe ya akieneza ujumbe wa bwenyenye huyo.

Crystler ni moja wapo ya magari "makubwa matatu" yanayotengenezwa nchini Amerika.

Hatua hii inajiri siku chache baada ya mcheshi huyo kutangaza kumuidhinisha Wanjigi kuwania urais akisema ndiye anayejali maslahi ya vijana.

Kupitia kampeni yenye kauli mbiu ‘Fagia Wote’, Omondi alisema Wanjigi anaelewa kamili kile vijana wanataka kwani ana uzoefu wa biashara ambao utawafaa vijana.

“Vijanaa tunahitaji rais mwenye anatujali. Vijanaa tunahitaji mtu fresh, sura mpya; mtu hajakua kwa ofisi. Vijanaa tunaneed rais mweye anaelewa biashara na mahitaji ya vijanaa. Vijanaa, tunahitaji Jimmy Wanjigi. Vijanaa tunaendorse Jimi Wanjigi, Eric Omondi ninaendorse Jimi Wanjigi,” Eric alisema.

Wanjigi ametangaza kuania urais kwa chama cha ODM na yuko tayari kwa kinyang’anyiro cha kutafuta atakaye peperusha bendera ya chama hicho.

Gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kakamega Wycliffe Oparanya pia wameonyesha ari ya kutaka tiketi ya ODM.

Kinara wa chama hicho Raila Odinga pia anatarajiwa kuania tiketi  ya chama hicho na wachanganuzi wengi wanasema ni yeye atakaye pewa tiketi hiyo.