COVID 19: Visa vipya 511 vyaripotiwa, wagonjwa 1,108 wamelazwa hospitalini

Muhtasari

•Kufikia sasa jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa nchini imefikia 243, 456 huku asilimia ya maambukizi kwa sasa ikiwa 7.9%.

•Kufikia sasa watu 2,255,214 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo  dhidi ya Corona huku 826,396 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imerekodi visa 511 vipya vya wagonjwa wa COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 6,434 ambao wamepimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita.

Kufikia sasa jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa nchini imefikia 243, 456 huku asilimia ya maambukizi kwa sasa ikiwa 7.9%.

Mtoto wa miezi kumi na mkongwe wa miaka 96 ni miongoni mwa wagonjwa wapya ambao wameripotiwa na wizara ya afya.

Kaunti ya Nairobi inaendelea kuongoza kwa maambukizi hivi leo ikiandikisha visa 93. Kiambu inafuata na visa 56, Nakuru 39, Nyeri 30 huku kaunti zingine zikiwa na visa chini ya 30.

Wagonjwa 1,018 wameweza kupona ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita,  810 wakiponea nyumbani huku 208 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 231, 958 wamewahi kupona maradhi hayo nchini.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 4902 baada ya vifo vingine 6 kuripotiwa leo.

Wagonjwa 1,617 wanaendelea kuhudumiwa hospitalini huku wengine 4,447 wakiwa wanahudumiwa manyumbani. Wagonjwa 148 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo  ya Corona

Kufikia sasa watu 2,255,214 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo  dhidi ya Corona huku 826,396 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.