COVID 19: Wagonjwa 1,600 wanahudumiwa hospitalini, 960 wapona

Muhtasari

•Mtoto wa mwaka mmoja ndiye mtu mdogo zaidi aliyepatikana na virusi hivyo katika kipindi hicho huku mkongwe wa miaka 101 akiwa mtu mzee zaidi kupatikana navyo.

Image: HISANI

Leo Kenya imerekodi visa 269 vipya vya wagonjwa wa COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 3,872 ambao wamepimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita.

Kufikia sasa jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa nchini imefikia 243, 725 huku asilimia ya maambukizi kwa sasa ikiwa 6.9%.

Mtoto wa mwaka mmoja ndiye mtu mdogo zaidi aliyepatikana na virusi hivyo katika kipindi hicho huku mkongwe wa miaka 101 akiwa mtu mzee zaidi kupatikana navyo.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa maambukizi hivi leo ikiandikisha visa 117. Kajiado inafuata na visa 20, Machakos 18, Nakuru 17 ,Meru 11, Uasin Gishu 11, Kitui 10 huku kaunti zingine zikiwa na visa chini ya 10.

Wagonjwa 960 wameweza kupona ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita,  895 wakiponea nyumbani huku 65 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 231, 958 wamewahi kupona maradhi hayo nchini.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 4906 baada ya vifo vingine 4 kuripotiwa leo.

Wagonjwa 1,600 wanaendelea kuhudumiwa hospitalini huku wengine 4,032 wakiwa wanahudumiwa manyumbani. Wagonjwa 148 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo  ya Corona

Kufikia sasa watu 2,262,968 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo  dhidi ya Corona huku 827,964 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.