Covid-19:Watu 204 wapatikana na corona,984 wapona,17 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 204 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,963 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 198 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa kigeni,102 ni wanaume huku 102 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Watu 204 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,963 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 198 ni wakenya ilhali 4 ni raia wa kigeni,102 ni wanaume huku 102 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 243,929 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.9%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,457,626.

Hata hivyo watu 17 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,923 ya walioaga dunia.

Aidha watu 984 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 233,902, 518 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 466 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,555 ambao wamelazwa hospitalini, 3,345 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 138  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).