Covid-19:Watu 451 wapatikana na corona huku 5 wakiaga dunia

Muhtasari
  • Watu 451 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,833 chini ya saa 24 zilizopita
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 436 ni wakenya ilhali 15 ni raia wa kigeni,244 ni wanaume huku 207 wakiwa wanawake
Image: HISANI

Watu 451 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,833 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 436 ni wakenya ilhali 15 ni raia wa kigeni,244 ni wanaume huku 207 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 244,380 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.6%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,464,459.

Hata hivyo watu 5 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,928 ya walioaga dunia.

Aidha watu 835 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 234,737, 770 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 65 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,559 ambao wamelazwa hospitalini, 3,427 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 122  katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).