Seneta Linturi aachiliwa kwa dhamana ya 200,000 baada ya kukanusha mashtaka ya jaribio la ubakaji dhidi yake

Muhtasari

•Mwanasiasa huyo pia alishtakiwa kwa kosa la kumshika mwanamke huyo vibaya bila idhini yake.

Seneta wa Meru Mithika Linturi
Seneta wa Meru Mithika Linturi
Image: ENOS TECHE

Habari na Carolyne Kubwa

Seneta wa Meru Mithika Linturi amekanusha mashtaka ya jaribio la ubakaji aliyosomewa katika mahakama ya Milimani siku ya Jumanne.

Mwanamke mmoja alishtaki Linturi kwamba aliingia ndani ya chumba cha wageni katika hoteli moja upande wa Nanyuki na kujaribu kumbaka.

Kulingana na karatasi ya mashtaka, Linturi alidaiwa kuingia ndani ya chumba cha hoteli ya Maiyan Villas mida ya saa tisa usiku na kujaribu kushiriki ngono na mwanamke wa miaka 36 bila idhini yake.

Mwanasiasa huyo pia alishtakiwa kwa kosa la kumshika mwanamke huyo vibaya bila idhini yake.

Hata hivyo Linturi amekanusha madai hayo mbele ya hakimu Martha Nanzushi na kuomba aachiliwe kwa dhamana ya haki.

Mahakama imekubali kumwachilia seneta huyo kwa dhamana ya shilingi laki mbili huku kesi hiyo ikitatarajiwa kutajwa tena mnamo Oktoba 26.