Makali ya corona: Watu 234 wapatikana na corona,492 wapona, 9 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,498,049
  • Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 4  ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 97
  • Hata hivyo watu 9 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,989 ya walioaga dunia
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imesajili visa 234 vipya vya maambukizi ya Covid-19  siku ya JUmapili kutoka kwa sampuni 3,737 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 231 ni wakenya ilhali 3 ni raia wa kigeni,118 ni wanaume huku 116 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 246,530na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.3 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,498,049.

Mgonjwa wa umri wa chini ana miaka 4  ilhali mwenye umri wa juu ana miaka 97.

Hata hivyo watu 9 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 4,989 ya walioaga dunia.

Aidha watu 492 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 237,295 452 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 40  wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 1,433 ambao wamelazwa hospitalini, 3,246 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 109 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,351,109.