Covid-19: Watu 37 waaga dunia huku 394 wakipatikana na corona

Muhtasari
  • Kiwango cha corona sasa ni 5.4%
  • Kutoka kesi 383 ni Wakenya wakati 11 ni wageni. Wanaume 213 wakati 181 ni wanawake
  •  
    Mgonjwa wa miaka ya chini ni mtoto wa miezi 2 wakati mzee ni miaka 102
Image: HISANI

Watu 394 wamepatikana na virusi vya maambukizi ya corona , kutokana na ukubwa wa sampuli ya 7,254 iliyojaribiwa katika masaa 24 iliyopita.

Kiwango cha corona sasa ni 5.4%.

Kutoka kesi 383 ni Wakenya wakati 11 ni wageni. Wanaume 213 wakati 181 ni wanawake.

Mgonjwa wa miaka ya chini ni mtoto wa miezi 2 wakati mzee ni miaka 102.

Jumla ya kesi zilizothibitishwa nchini ni 248,069 kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 2,527,861. 

Aidha watu 414 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 239,298, 367 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 47 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kwa habari za kuhuzunisha watu 37 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,082 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 1,241 ambao wamelazwa hospitalini, 2,707 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 87 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).