COVID 19: Wagonjwa 1220 wamelazwa hospitalini; Vifo 14 vyaripotiwa

Muhtasari

•Kufikia sasa jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa nchini imefikia 248,392 huku asilimia ya maambukizi kwa sasa ikiwa 5.8%.

•Mtoto wa miezi miwili na mkongwe wa miaka 104 ni miongoni mwa wagonjwa wapya ambao wameripotiwa na wizara ya afya.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imerekodi visa 323 vipya vya wagonjwa wa COVID 19 kutoka kwa sampuli ya watu 5,606 ambao wamepimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita.

Kufikia sasa jumla ya visa ambavyo vimewahi kuripotiwa nchini imefikia 248,392 huku asilimia ya maambukizi kwa sasa ikiwa 5.8%.

Mtoto wa miezi miwili na mkongwe wa miaka 104 ni miongoni mwa wagonjwa wapya ambao wameripotiwa na wizara ya afya.

Hivi leo kaunti ya Nandi inaongoza kwa maambukizi ikiripoti visa 71. Nairobi inafuata na visa 41, Nakuru 30, Nyeri 22 huku kaunti zingine zikiwa na visa chini ya 20.

Wagonjwa 432 wameweza kupona ndani ya kipindi cha masaa 24 ambayo yamepita,  387 wakiponea nyumbani huku 45 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 239,730 wamewahi kupona maradhi hayo nchini.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 5096 baada ya vifo vingine 14 kuripotiwa leo.

Wagonjwa 1220 wanaendelea kuhudumiwa hospitalini huku wengine 2694 wakiwa wanahudumiwa manyumbani. Wagonjwa 148 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo  ya Corona

Kufikia sasa watu 2,713,427 wameweza kupokea angalau dozi moja ya chanjo  dhidi ya Corona huku 886,760 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.