COVID 19: Wagonjwa 505 wapata afueni, Vifo 6 vyaripotiwa

Muhtasari

•Kufikia sasa watu 2,724, 742 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 888, 615 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.

Image: HISANI

Wizara ya afya imetangaza visa vipya  69 nchini kutoka kwa sampuli ya watu 1,414 ambao wameweza kupimwa ndani ya kipindi cha masaa 24 ambacho kimepita. Hii inaashiria kwamba asilimia ya maambukizi nchini kwa sasa ni 4.9%.

Kufikia sasa Kenya imewahi kurekodi visa 248,461 kutoka kwa jumla ya vipimo 2,54,881 ambavyo vimewahi kufanywa tangu mwanzo wa janga la Corona.

Nairobi imeripoti visa 24, Meru 12, Nakuru 4, Muranga 3, Makueni 3, Taita Taveta 3 huku Kakamega, Mombasa , Kiambu, Nyeri, Uasin Gishu na Isiolo zikiandikisha visa viwili kila kaunti.

Wagonjwa 505 wameweza kupona, 466 wakiponea nyumbani huku 39 wakipona kutoka vituo mbalimbali vya afya nchini. Kufikia sasa watu 240, 235 wamewahi kupona maradhi hayo.

Idadi ya vifo nchini kutokana na COVID 19 imefikia 5102 baada ya vifo 6 zaidi kuripotiwa leo.

Kwa sasa wagonjwa 1209 wanahudumiwa hospitalini huku wengine 2,633 wakipokea matibabu kutoka manyumbani kwao. Wagonjwa 87 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Chanjo ya Corona

Kufikia sasa watu 2,724, 742 wamepokea angalau dozi moja ya chanjo dhidi ya Corona huku 888, 615 wakiwa wamepokea dozi zote mbili.