Covid-19:Watu 437 wapona corona,54 wapatikana na corona,7 waaga dunia

Muhtasari
  • Watu 54 wamepatikana na virusi vya maambukizi ya corona , kutokana na ukubwa wa sampuli ya 2,501  zilizopimwa katika masaa 24 iliyopita
  • Kiwango cha corona sasa ni 2.2%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Watu 54 wamepatikana na virusi vya maambukizi ya corona , kutokana na ukubwa wa sampuli ya 2,501  zilizopimwa katika masaa 24 iliyopita.

Kiwango cha corona sasa ni 2.2%.

Kutoka kesi 52 ni Wakenya wakati 2 ni wageni. Wanaume 24 wakati 30 ni wanawake.

Mgonjwa wa umri wa chini ni mtoto wa miaka 2 wakati mzee ni miaka 93.

Jumla ya kesi zilizothibitishwa nchini ni 248,515 kutoka kwa idadi jumla ya sampuli 2,537,382. 

Kulingana na kaunti;Nairobi 22, Machakos 7, Murang’a 4, Nakuru 4, Uasin Gishu 3, Kajiado 2, Nyeri 2, Wajir, Baringo, Kakamega, Kiambu, Nandi, Kirinyaga, Kisii, Meru, Mombasa and Trans Nzoia kisa 1 mtawalia.

Aidha watu 437 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 240,672, 314 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 123 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kwa habari za kuhuzunisha watu7 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,109 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 1,126 ambao wamelazwa hospitalini, 2,586 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 73 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).