Marekani yapatia Kenya msaada wa dozi 210,600 za chanjo ya Pfizer

Muhtasari

•Ndege iliyokuwa imebeba chanjo hizo ilitua katika uwanja wa ndege wa JKIA  asubuhi ya Jumanne na kulakiwa na afisa wa afya katika ubalozi wa Marekani nchini, Dkt Douglas Shaffer.

Dkt Douglas Shaffer akichunguza dozi 210,600 za Pfizer katika uwanja wa JKIA
Dkt Douglas Shaffer akichunguza dozi 210,600 za Pfizer katika uwanja wa JKIA
Image: US EMBASSY

Serikali ya Marekani imepatia Kenya msaada wa dozi 210,600 za chanjo dhidi ya COVID-19 aina ya Pfizer.

Ndege iliyokuwa imebeba chanjo hizo ilitua katika uwanja wa ndege wa JKIA  asubuhi ya Jumanne na kulakiwa na afisa wa afya katika ubalozi wa Marekani nchini, Dkt Douglas Shaffer.

"Marekani kupitia kwa USAID na kituo cha kuthibiti na kuzuia maradhi cha Marekani pia imewekeza shilingi milioni 495 ili kusaidia kusambazwa kwa chanjo nchini Kenya" Ubalozi wa Marekani ulitangaza.

Kufikia sasa Marekani imepatia Kenya msaada wa takriban dozi milioni 3 za chanjo dhidi ya maradhi ya COVID 19.

Alipokuwa anatangaza kuwasili kwa dozi hizo, Dkt Shaffer amesihi Wakenya kujitokeza kupokea chanjo ili kujilinda na kulinda wenzao.