Makali ya corona:Watu 291 wapatikana na corona,308 wapona,5 waaga dunia

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 282 ni wakenya ilhali 9 ni raia wa kigeni,160 ni wanaume huku 131 wakiwa wanawake
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,725 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.5 %
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Kenya imesajili visa 291 vipya vya maambukizi ya Covid-19 siku ya Ijumaa kutoka kwa sampuni 6,501 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 282 ni wakenya ilhali 9 ni raia wa kigeni,160 ni wanaume huku 131 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 249,725 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 4.5 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,562,723.

Hata hivyo watu 5 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,128 ya walioaga dunia.

Aidha watu 308 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 241,828,208 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 100 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Kuna wagonjwa 963 ambao wamelazwa hospitalini, 2,078 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 61 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,811,136