Covid-19:Jumla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,886,630,77 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 77 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,415 chini ya saa 24 zilizopita
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: MoH

Kenya imesajili visa 77 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 2,415 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 70 ni wakenya ilhali 7 ni raia wa kigeni,42 ni wanaume huku 35 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,191 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.2 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,575,024.

Aidha watu 322 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 242,557,287 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 35 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo mtu 1 ameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,141 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 914 ambao wamelazwa hospitalini, 1,979 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 56 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,886,630.