Kafyu ya kitaifa kusalia kwa kipindi cha siku 30 zaidi- Waziri Mutahi Kagwe

Muhtasari

•Alipokuwa anazungumza asubuhi ya Jumatatu, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kuwa kipindi cha siku 30 ambacho kimeongezwa kitatumiwa kuchanja watu zaidi.

Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Mikakati iliyowekwa ili kuthibiti maambukizi ya virusi vya Corona nchi itaendelea kuzingatiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja zaidi.

Alipokuwa anazungumza asubuhi ya Jumatatu, waziri wa afya Mutahi Kagwe alisema kuwa kipindi cha siku 30 ambacho kimeongezwa kitatumiwa kuchanja watu zaidi.

Kagwe alisema kwamba asilimia ya maambukizi nchini ingali juu ya asilimia ya 5% ambayo imependekezwa na WHO  kutimia kabla ya kulegezwa kwa mikakati iliyowekwa.

"Tunahiatji siku 30 ambazo tumeongeza ili tuweze kuchanja watu wengi zaidi kama iwezekanavyo. Tunapoelekea kwenye sherehe za Krisimasi tunafaa kuhakikisha kuwa watu wengi zaidi nchini wameweza kupokea chanjo" Waziri kagwe amesema.

Miongoni mwa mikakati ambayo tayari ilikuwa imewekwa ni pamoja na kafyu ya kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi asubuhi, marufuku ya mikusanyiko ya watu, marufuku ya mikutano ya hadhara kati ya mikalati mingine.