Gavana Lonyang'apuo azindua chama chake baada ya kugura KANU

Muhtasari

•Kupitia kwa tangazo ambalo lilichapishwa kwenye gazeti la taifa, msajili wa vyama vya kisiasa alipatia watu ambao wangependa kupinga kusajiliwa kwa chama hicho hadi siku ya Ijumaa za kuwasilisha ombi.

Image: FACEBOOK// PROF JOHN LONYANGAPUO

Gavana wa West Pokot John Lonyang'apuo ni mwanasiasa wa hivi karibuni kuzindua chama chake tunapokaribia chaguzi kuu za mwaka ujao.

Gavana huyo ambaye alichagulia kwa tikiti ya chama cha KANU ametangaza kuzinduliwa kwa chama cha Kenya Union Party(KUP) ambacho alama yake itakuwa alama mbili za 'Tick' (✔️✔️)

"Habari Wakenya. Ni siku mpya! Hapa naleta chama kipya cha siasa, Kenya Union Party(KUP). Alama (✔️✔️) na slogan UMOJA WETU. " Lonyangapuo alitangaza siku ya Jumanne kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hatua hii inakuja miezi michache tu baada ya mwanasiasa huyo kugura chama cha KANU akidai kuwa kilikuwa kinafadhaisha uongozi wake katika kaunti ya West Pokot.

Kupitia kwa tangazo ambalo lilichapishwa kwenye gazeti la taifa, msajili wa vyama vya kisiasa alipatia watu ambao wangependa kupinga kusajiliwa kwa chama hicho hadi siku ya Ijumaa za kuwasilisha ombi. 

Lonyangapuo anatazamia kutumia chama cha KUP kutetea kiti chake cha ugavana mwaka ujao.