Makali ya corona: Watu 189 wapatikana na corona,207wapona,9 waaga dunia

Muhtasari
  • Kenya imesajili visa 189 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,367 chini ya saa 24 zilizopita
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Kenya imesajili visa 189 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,367 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 182 ni wakenya ilhali 7 ni raia wa kigeni,90 ni wanaume huku 99 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,380 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 3.0 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,581,391.

Aidha watu 207 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 243,064,117 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 90 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo mtu 9 ameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,150 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 894 ambao wamelazwa hospitalini, 1,961 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 51 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).

JUmla idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 3,935,671.