Makali ya corona:Watu 25 waaga dunia kutokana na corona asimilia ya corona ni 2.7%

Muhtasari
  • Hata hivyo mtu 25 ameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,175 ya walioaga dunia
  • Kuna wagonjwa 865 ambao wamelazwa hospitalini, 1,906 wamejitenga nyumbani
Waziri wa afya Mutahi Kagwe
Image: MoH

Kenya imesajili visa 130 vipya vya maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 4,869 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 127 ni wakenya ilhali 3 ni raia wa kigeni,74 ni wanaume huku 56 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 250,510 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.7 %.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,586,260

Aidha watu 222 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 243,286,169 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 53 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo mtu 25 ameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,175 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 865 ambao wamelazwa hospitalini, 1,906 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 56 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICI).