Ni marufuku kwa polisi kuvalia nguo za raia na kutumia probox kufanya operesheni jijini Nairobi

Muhtasari

•Polisi amabo wanafanya operesheni kama  vile kufungwa kwa baa, ukaguzi wa leseni na kukamata washukiwa wanapaswa kuvalia sare rasmi ya bluu kila wakati.

•Polisi pia wameonywa dhidi ya kufanya majukumu yoyote ya polisi nje ya eneo ambalo wametengewa kufanya kazi. Hatua kali itachukuliwa kwa afisa  yeyote ambaye atakiuka maagizo hayo.

THE STAR

Katika juhudi za kukabiliana na ukora miongoni mwa maafisa wa polisi, kamanda wa polisi katika eneo la Nairobi Augustine Nthumbi ametoa sheria kali kwa maafisa wanaofanya kazi jijini.

Polisi amabo wanafanya operesheni kama  vile kufungwa kwa baa, ukaguzi wa leseni na kukamata washukiwa wanapaswa kuvalia sare rasmi ya bluu kila wakati.

Nthumbi amepiga marufuku uvaliaji wa nguo za raia wa kawaida na matumizi ya magari aina ya probox wakati polisi wanafanya operesheni.

"Utumizi ya polisi ambao wamevalia manguo ya raia na kuabiri probox umepigwa marufuku na iwapo kesi kama hiyo itaripotiwa  itakuwa kesi ya operesheni haramu  na wizi kwa raia ambayo ni uhalifu" Nthumbi aliagiza.

Polisi pia wameonywa dhidi ya kufanya majukumu yoyote ya polisi nje ya eneo ambalo wametengewa kufanya kazi. Hatua kali itachukuliwa kwa afisa  yeyote ambaye atakiuka maagizo hayo.

Ntumbi amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kazi ya polisi kutekelezwa kwa njia ya utaalamu wa hali ya juu na kuwaagiza raia kuwa makini na kuripoti polisi wakora.

"Kazi ya polisi inafaa kufanywa kwa utaalam kwa kutumia rasilimali halali. Ambapo gari za kibinafsi zitatumika kufanya majukumu ya polisi, OCS atalazimika kueleza. Lazima tukuze biashara sio kuzidhalilisha. Wanainchi kaa rada na mripoti polisi wakora katika eneo lenu" Ntumbi alisema.