Mudavadi aongoza OKA kwa mashauriano na wakfu wa Mt Kenya

Muhtasari

• Mkutano huu ujairi siku chache baada ya viongozi wa wakfu wa Mt Kenya kukutana kinara wa ODM Raila Odinga.

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Kinara wa ANC Musalia Mudavadi
Image: HISANI

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi ameongoza wanachama wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA) Kalonzo Musyoka wa Wiper, Gideon Moi wa Kanu na Moses Wetangula wa Ford Kenya katika mkutano na wanachama wa wakfu wa Mlima Kenya (Mt Kenya Foundation).

Mkutano huu ujairi siku chache baada ya viongozi wa wakfu wa Mt Kenya kukutana kinara wa ODM Raila Odinga.

Katika hotuba yake aliyekuwa waziri katika serikali ya hayati rais Daniel Moi,  Cyrus Jirongo alitoa wito kwa viongozi wa wakfu huo kutopendelea mgombeaji yeyote kwa sasa na badala yake kuwapa wote nafasi sawa kuuza sera zao.

Kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula  alisema kwamba kama wanasiasa watahakikisha kwamba kila mkenya anaishi bila hofu katika kila pembe ya taifa la Kenya.

Alisema hakuna anayefaa kutishia mwingine kwa sababu za kisiasa.