Mwalimu ahukumiwa kifungo cha miaka 20 kwa kunajisi mwanafunzi wa darasa la 6

Polisi walipeleka mlalamishi hospitalini ambapo alipimwa na akapewa ushauri.

Muhtasari

•Mahakama iliarifiwa kwamba baba ya mhasirirwa ambaye alikuwa mlevi alikuwa amemuachia Mwangi achunge bintiye kwa kipindi cha nusu mwaka.

•Mhasiriwa alifunguka na kueleza kuwa Mwangi alikuwa anamdhulumu kingono tangu alipoanza kuishi naye na kumtishia dhidi ya kufichua jambo hilo.

Mwalimu Fredrick Mwangi ambaye alipatikana na hatia ya kunajisi msichana wa miaka 13
Mwalimu Fredrick Mwangi ambaye alipatikana na hatia ya kunajisi msichana wa miaka 13
Image: ENOS TECHE

Mwalimu mmoja anayedaiwa kunajisi mwanafunzi wa miaka 13 mnamo mwaka wa 2016 alihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani siku ya Jumatano.

Fredrick Mwangi, 45, alihukumiwa kifungo hicho na hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani David Ndungi baada ya mahakama kumpata na hatia. Ndungi alisema kwamba upande wa mahakama ulithibitisha kesi yao dhidi yake.

Alipokuwa anatoa hukumu yake, hakimu aisema kwamba hukumu hiyo  ndiyo ya chini zaidi kama ilivyopendekezwa na sheria.

Mwangi alishutumiwa kunajisi mtoto wa darasa la sita ambaye alikuwa anaishi naye kwa nyumba yake katika mtaa wa Mathare, Nairobi mnamo Machi 2016.

Mahakama iliarifiwa kwamba baba ya mhasirirwa ambaye alikuwa mlevi alikuwa amemuachia Mwangi achunge bintiye kwa kipindi cha nusu mwaka. Mwangi ameoa na ana watoto wawili.

Mlezi wa msichana huyo ambaye ni afisa wa polisi alimchukua kutoka kwa Mwangi akampeleka katika kituo cha polisi cha Central.

"Alipelekwa katika shule mbili tofauti ila angecha na kurejea kwa Mwangi na haikueleweka mbona  alipendelea kukaa pale" Mahakama iliarifiwa.

Mnamo Oktoba 13, 2016 mhasiriwa alichukua nguo zake na kuenda kwa Mwangi ambapo alipata bintiye kwani mfungwa pamoja na mkewe walikuwa shuleni tayari.

Wenye nyumba waliporejea nyumbani jioni walimpata msichana huyo akiwa amevalia sare ya shule.

Mlezi wa mlalamishi alimpigia mshtakiwa simu na akathibitisha kwamba alikuwa kwake. Alimwambia Mwangi ampeleke msichana huyo nyumbani kwake katika kituo cha polisi cha Central na wakampeleka wakiwa na mkewe.

Msichana huyo alihojiwa ikiwa kulikuwa na uhusiano wowote wa mapenzi kati yake na mshtakiwa ama mtu yeyote upande wa Mathare ila akakunusha.

Mnamo Oktoba 15 polisi walipeleka mlalamishi hospitalini ambapo alipimwa na akapewa ushauri. 

Alifunguka na kueleza kuwa Mwangi alikuwa anamdhulumu kingono tangu alipoanza kuishi naye na alimtishia dhidi ya kufichua jambo hilo.

(Utafsiri: Samuel Maina)