Jamaa aua mwenzake kwa kisu juu ya mwanadada ambaye walimpenda wote wawili Bungoma

Muhtasari

•Oliver Wafula anaripotiwa kuua Titus Wamalwa kwa kutumia kisu asubuhi ya Jumatatu katika eneo la Bumula walipokuwa wanakwaruzana juu ya mwanadada aliyetambulishwa kama Njoki. 

•Inaripotiwa kwamba marehemu ambaye inaaminika alikuwa na ujuzi wa kucheza ndondi alimpiga Wafula ngumi vibaya kabla ya mshukiwa  kuchukua kisu na kukitumia kumdunga kifuani alipoona kuwa ameelewa nguvu

Crime scene
Crime scene

Polisi katika kaunti ya Bungoma wanamzuilia jamaa mmoja anayedaiwa kuua mwenzake kufuatia mzozo juu ya mwanamke.

Oliver Wafula anaripotiwa kuua Titus Wamalwa kwa kutumia kisu asubuhi ya Jumatatu katika eneo la Bumula walipokuwa wanakwaruzana juu ya mwanadada aliyetambulishwa kama Njoki. 

Kulingana na DCI, wawili hao walikuwa wamekutana nyumbani kwa Njoki ambaye kila mmoja wao alimtaka ndipo vita vikaanza.

Inaripotiwa kwamba marehemu ambaye inaaminika alikuwa na ujuzi wa kucheza ndondi alimpiga Wafula ngumi vibaya kabla ya mshukiwa  kuchukua kisu na kukitumia kumdunga kifuani alipoona kuwa ameelewa nguvu.

Wamalwa alikufa papo hapo kutokana na jeraha mbaya la kisu naye mshukiwa kuona alichokuwa amekitenda akaenda mafichoni.

Baada ya kumsaka mshukiwa kwa masaa kadhaa wapelelezi  walimkamata katika soko ya Kimwanga alipokuwa anajaribu kukimbia mji wa Bumula.

Kisu ambacho kilitumika kutekeleza mauaji kilipatika na  kinahifadhiwa ili kitumike kama ushahidi mahakamani.