Makali ya corona:Wagonjwa 640 wamelezwa,186 wapatikana na corona

Muhtasari
  • Watu 186 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,965 chini ya saa 24 zilizopita
Image: HISANI

Watu 186 wamepatikana na  maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,965 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 179 ni wakenya ilhali 7 ni raia wa kigeni,99 ni wanaume huku 87 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,669 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.7%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,624,665.

Vile vile watu 189 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 244,935,135 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 54 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Hata hivyo watu 4 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,202ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 640 ambao wamelazwa hospitalini, 1,631 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 35 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 4,340,511.