Covid-19: Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 4,406,433,8 waaga dunia

Muhtasari
  • Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,803 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.2%
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: HISANI

Watu 134 wamepatikana na maambukizi ya Covid-19 kutoka kwa sampuni 6,047 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo mapya wagonjwa 128 ni wakenya ilhali 6 ni raia wa kigeni,70 ni wanaume huku 64 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 251,803 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 2.2%.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 2,630,712.

Vile vile watu 142 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 245,077,93 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani ilhali 49 wameruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti.

Aidha watu 8 wameaga dunia kutokana na virusi vya corona, na kufikisha idadi jumla ya 5,210 ya walioaga dunia.

Kuna wagonjwa 612 ambao wamelazwa hospitalini, 1,608 wamejitenga nyumbani.

HUku hayo yakijiri kuna wagonjwa 31 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 4,406,433.