Jamaa 45 atoroka baada ya kumbaka mamake 90, Mbooni

Madaktari walithibitisha kwamba alikuwa amebakwa.

Muhtasari

• Kulingana na idara ya DCI mshukiwa Patrick Mumo  alikwenda mafichoni punde baada ya kutekeleza unyama huo.

Pingu
Image: Radio Jambo

Maafisa kutoka kitengo cha upelelezi wameanzisha msako kumtafuta mshukiwa aliyembaka mama yake mwenye umri wa miaka 90 siku ya Mashujaa Day, katika eneo la Mbooni kaunti Makueni.

Kulingana na idara ya DCI mshukiwa Patrick Mumo  alikwenda mafichoni punde baada ya kutekeleza unyama huo.

Mama huyo katika miaka yake ya machweo alipatikana katika chumba chake cha kulala na mwanawe mkubwa akilia kwa maumivu makali, akilalamika kuwa na maumivu ya kiuno.

Alisimulia huku akidondokwa na machozi masaibu aliyopitia katika mikono ya mtoto wake kitinda mimba mwenye umri wa miaka, 45.

Kulingana na mama huyo mshukiwa aliingia chumbani mwake kwa nguvu mwendo wa saa mbili usiku akiwa amelala na kumfanyia kitendo hicho cha kinyama.

Alikimbizwa katika hospitali ya Kaunti Ndogo ya Kisau akiwa katika hali mbaya ambapo anaendelea kupokea matibabu.

Madaktari walithibitisha kwamba alikuwa amebakwa. Maafisa wa upelelezi wanamemtaka mshukiwa Patrick Mumo kujitokeza mapema ili akabiliwe kisheria.