Polisi wanaodaiwa kufanikisha kutoroka kwa muuaji Masten Wanjala wakanusha mashtaka

Muhtasari

•Watatu hao ambao ni Philip Mbithi, Boniface Mutuma na Precious Mwinzi walikanusha mashtaka ya kusaidia mahabusu kutoroka na ya kutowajibika kazini ambayo yaliwakabili.

•Hakimu Bernard Ochoi aliamuru waachiliwe kwa dhamana ya shilingi 300,000 huku akiagiza kesi hiyo itajwe tena mnamo tarehe 4 Novemba.

Washukiwa Philip Mbithi, Kamakia Mutuma Boniface na Preciouss Mbithi mbele ya Hakimu Jane Kamau mnamo Oktoba 14
Washukiwa Philip Mbithi, Kamakia Mutuma Boniface na Preciouss Mbithi mbele ya Hakimu Jane Kamau mnamo Oktoba 14
Image: ANNETTE WAMBULWA

Habari na Annette Wambulwa

Maafisa watatu wa polisi ambao walikuwa katika zamu wakati muuaji aliyekiri kuua watoto zaidi ya kumi  Masten Wanjala  alitoroka walifikishwa mahakamani asubuhi ya Ijumaa.

Watatu hao ambao ni Philip Mbithi, Boniface Mutuma na Precious Mwinzi walikanusha mashtaka ya kusaidia mahabusu kutoroka na ya kutowajibika kazini ambayo yaliwakabili.

Inadaiwa kwamba watatu hao walishirikiana kusaidia Wanjala kutoroka kizuizinikatika kituo cha polisi cha Jogoo mnamo Oktoba 12.

Watatu hao pia walishtakiwa kwa kosa la kutowajibika katika kazi yao ya kuzuia mshukiwa wa mauaji kutoroka kama walivyotakikana na s

Kupitia kwa wakili wao Danstan Omari, maafisa hao waliomba kuachiliwa kwa dhamana inayofaa na kuomba wasaidiwe na karatasi za mahakama ambazo zitatumika wakati wa kesi yao.

Hakimu Bernard Ochoi aliamuru waachiliwe kwa dhamana ya shilingi 300,000 huku akiagiza kesi hiyo itajwe tena mnamo tarehe 4 Novemba.

Hapo awali upande wa mashtaka ulikuwa umeambia hakimu Jane Kamau kwamba uchunguzi ulikuwa umekamilika na kudai kwamba kesi ilikuwa tayari kuendelea.

Watatu hao walikuwa wameachiliwa kwa dhamana ya 100,000 wiki iliyopita na wamekuwa wakiripoti kwa afisa aliyekuwa anaongoza uchunguzi.