Mwanamke na bintiye wa miezi 6 wazuiliwa kufuatia mauaji ya mumewe Nairobi

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo Novemba 10

Muhtasari

•Inaripotiwa kwamba Wigama amekuwa akiishi na marehemu mumewe kwa kipindi  cha miaka mitano ambayo imepita na tayari walikuwa wamejaliwa watoto wawili.

•Bi Wigama aliporejea nyumbani mabishano kati yake na mumewe yaligeuka kuwa vita ambayo ilipelekea mshukiwa kumdunga mumewe kifuani.

Crime scene
Crime scene

Mwanamke mmoja na mtoto wake mwenye umri wa miezi mitatu wanazuiliwa katika gereza la wanawake la Lang'ata kuhusiana na mauaji ya mume wake jijini Nairobi.

Siku ya Ijumaa mpelelezi Peter Njonjo aliambia mahakama kwamba Celestine Wigama anatuhumiwa kuua mumewe Dennis Watangu mnamo Oktoba 17.

Inaripotiwa kwamba Wigama amekuwa akiishi na marehemu mumewe kwa kipindi  cha miaka mitano ambayo imepita na tayari walikuwa wamejaliwa watoto wawili.

Njonjo alisema kwamba wanandoa hao wawili walikuwa ndani ya nyumba yao wakati mzozo mkubwa uliibuka kati yao.

Alieleza kwamba wawili hao walikuwa wanazozana kuhusu binti yao mkubwa ambaye inadaiwa amekuwa akiharibu vitabu vyake vya kuandikia.

Mabishano hayo yalichochea Wigama kuondoka pale nyumbani na kuenda kwingine ili ampatie mumewe nafasi ya kutulia.

Bi Wigama aliporejea nyumbani mabishano kati yake na mumewe yaligeuka kuwa vita ambayo ilipelekea mshukiwa kumdunga mumewe kifuani.

Mpelelezi Opondo aliomba mahakama ipatie polisi ruhusa ya kumzuia mshukiwa kwa kipindi cha siku 14 zaidi ili kumpa nafasi ya kukamilisha uchunguzi.

Alieleza kwambabado hakuwa amepata nafasi ya kumpeleka mshukiwa kufanyiwa vipimo vya kiakili, DNA na kukabisdhi ripoti ya uchunguzi kwa DPP ili apate ushauri.

Njonjo alisema kwamba hatua ya kuweka mtoto mbali na mama yake ingemnyima haki zake kama mtoto.

"Huyu ni mtoto ambaye hana hatia ambaye haki zake zinafaa kulindwa kwa njia zote" Njonjo alisema. 

Hakimu aliagiza mtoto apelekwe hospitalini kuona kwamba hali yake ya afya ilikuwa mbaya.

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo Novemba 10.

(Utafsiri: Samuel Maina)