Familia ya Masten Wanjala aliyekiri kuua watoto zaidi ya 10 yakataa mwili wake

Familia imesema haitamzika kwasababu inahofia kupata laana

Muhtasari

•Familia hiyo iliamua hata kukwepa kushiriki uchunguzi wa mwili wa mtoto wao kwa njia ya DNA uliofanywa na maafisa wa uchunguzi wa mwili kwa kuogopa laana.

•Kabla ya kifo chake Masten Wanjala alikiri binafsi kuwauwa watoto 10 katika kipindi cha miaka mitano.

Mshukiwa Masten Milimu Wanjala
Image: DCI

Familia ya mshukiwa sugu wa mauaji ya watoto aliyekiri ambaye aliuliwa kwao baada ya kutoroka kutoka mahabusu ya polisi imemkana.

Familia ya Masten Wanjala imesema haitamzika kwasababu inahofia kupata laana. Familia hiyo iliamua hata kukwepa kushiriki uchunguzi wa mwili wa mtoto wao kwa njia ya DNA uliofanywa na maafisa wa uchunguzi wa mwili kwa kuogopa laana.

Naibu Chifu wa Mukhweya Abiud Musungu alisema kuwa familia ya Wanjala ilikataa kupokea simu kutoka kwa maafisa ili wachukuliwe vipimo vya vinasaba-DNA na kumzika mtoto wao huyo wa kiume.

Chifu huyo amesema huenda serikali ikalazimika kumuua mshukiwa huyo wa mauaji iwapo familia itaendelea kuwa na msimamo wa kumkana.

Jirani wa Wanjala, Davis Wafula, alisema kuwa kama ukoo hawakutaka kujihusisha naye kwasbabu aliwaaabisha . “Tunaogopa iwapo tutamzika, sisi , kama ukoo, tunaweza kuonekana kama wauaji ,” alinukuliwa na vyombo vya habari Wafula akisema.

Masten Wanjala, aliyekuwa na umri wa miaka 20, alipatikana katika nyumba iliyopo katika mji wa Bungoma magharibi mwa nchi hiyo, baada ya kutoroka mahabusu ya polisi Nairobi na kupigwa hadi kufa na wanakijiji wenye hasira.

Kabla ya kifo chake Masten Wanjala alikiri binafsi kuwauwa watoto 10 katika kipindi cha miaka mitano.

Pia alikiri kuwavuta na wakati mwingine hata kunywa damu yao.

Aliripotiwa kurudi katika nyumba ya wazazi wake ambao walikuwa tayari wamemkataa- na hatimaye alipigwa na kunyongwa na majirani ambao walibaini kuwa alikuwa pale, zilisema taarifa za vyombo vya habari nchini Kenya